• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Busokelo District Council
Busokelo District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Busokelo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Adminstration
    • Organization Structure
    • Departments
      • Adminstration and Human Resource
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Health
      • Water
      • Sanitation and Environment
      • Agriculture, Irrigation and Cooperatives
      • Livestock and Fisheries
      • Development and Social Walfare
      • Land and Natural Resouces
      • Construction, Fire and Works
    • Units
      • Internal Audit
      • Bee Keeping
      • Election
      • Legal
      • Ict
      • Procurement and Supplies
  • Investment Oppotunities
    • Tourism
    • Agricultural
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • Councilors list
    • Standing Committee
      • Finance Planning and Adminstration
      • Economy Works and Environment
      • Education Health and Water
      • CMAC
      • Ethics committee
    • Schedules
      • Councilors schedule meetings
      • Chairperson schedule
  • Projects
    • Planned projects
    • On going projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Acts
    • Customer service contrct
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Kilimo

1.0 Utangulizi.

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina ukubwa wa eneo la hekta 96,914.0 (969.14 km2). Eneo lifaalo kwa kilimo ni hekta 49,389.67 na eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 43,569.76 sawa na asilimia 88.21 ya eneo linalofaa kwa Kilimo. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina jumla ya kaya zinazojishughulisha na kilimo 24,133 zenye wastani wa wakulima 72,399. 

 Kanda za Kilimo:

Halmashauri ya Busokelo imegawanyika katika kanda kuu tatu za kilimo, ukanda wa Chini, Kati na Juu. Katika kanda hizo tatu zinatofuatia kwa tabia ya hali ya hewa na mazao yanayolimwa kama ifuatavyo;

Ukanda wa chini: 

Unaundwa na Kata za Kisegese, Kambasegela, Itete, Lufilyo na sehemu ya kata ya Lupata katika vijiji vya Ntapisi na Bwibuka. Ukanda huu ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya mpunga, mahindi, mihogo, maharage, mbaazi, kokoa na matunda mbalimbali. Pia wakulima wa maeneo haya hufuga ng’ombe wa kienyeji (asili), mbuzi, nguruwe nk. Zana zitumikazo katika ukanda huu ni jembe la kukokotwa na maksai kwa 90%, pawatila kwa 10% na kwa upande mwingine jembe la mkono hutumika kwa 100%.

Hali ya hewa:

Ukanda huu ni wa joto na mvua za wastani kati ya milimita 800 – 900 kwa mwaka na kipindi kirefu ni cha ukame hivyo kilimo cha umwagiliaji kimepewa umuhimu mkubwa.

Miundombinu ya umwagiliaji:

Halmashauri ya wilaya ya Busokelo ina jumla ya skimu za umwagiliaji 12 ambazo ziko katika hatua tofauti tofauti za uboreshaji kama ifuatavyo; skimu 4 zimeboreshwa. Kifunda (Kata ya Lufilyo), Kisegese na Kasyabone (Kata ya Kisegese) na Mbambo (Kata ya Kambasegela).

Skimu 2 mbili uboreshaji unaendelea; Katelantaba (Kata ya Ntaba na K/segela) na Mbaka (Kata ya K/segela na Ntaba).

Skimu 3 zimefanyiwa upembuzi yakinifu; Ndola na Katungila (Kata ya Lufilyo) na Kilugu (Kata ya Itete). Skimu 3 bado hazijaanza kufanyiwa uboreshaji (mifereji ya asili inatumika). Skimu hizo ni; Lusungo, Mwabuke na Ipyana zote zipo kata ya Lufilyo.

Skimu zote zitachangia eneo la umwagiliaji lipatalo ha 2800 uboreshaji ukikamilika. Mpaka sasa eneo linalo mwagiliwa ni ha 1183 sawa na asilimia 42.25.

Ukanda wa kati:

Unaundwa na Kata za Lwangwa, Kabula na Sehemu Kata ya Lupata katika vijiji vya Lupata, Mpanda na Nsoso Ukanda huu kwa sehemu kubwa umefunikwa na mazao ya kudumu kama migomba, kahawa, chai, miwa nk. Pia mazao mbalimbali ya msimu hulimwa katika ukanda huu kama mahindi, maharage, karanga, viazi vitamu, viazi mviringo, mihogo, mboga, mbogamboga na matunda mbalimbali.

Wakulima wa maeneo haya hujishughulisha pia na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na wa kienyeji kwa kiasi kidogo, nguruwe, mbuzi wa maziwa nk. Jembe la mkono hutawala katika ukanda huu kwa 98.6% na sehemu iliyobaki, zana za kukokotwa na wanyama na matrekta.

Ukanda wa juu:

Ukanda huu unaundwa na Kata za Mpombo, Isange, Kandete na Luteba. Ukanda huu ni maarufu kwa kilimo cha viazi mviringo, mahindi, njegere, mazao ya bustani, na matunda. Wakulima wa maeneo haya pia ni wafugaji wa ng’ombe wa maziwa, nguruwe, mbuzi, kuku nk. Zana za kilimo zitumikazo katika ukanda huu ni jembe la mkono 97% na matrekta 3%.

Announcements

  • Tangazo la Nafasi za Kazi April 09, 2018
  • TANGAZO LA BODI YA MIKOPO January 19, 2018
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA January 19, 2018
  • Matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE) - 2017 January 31, 2018
  • View All

Latest News

  • Stop misleading statements of the President-Ngilangwa

    April 24, 2018
  • Distribute electricity house to house – Minister of energy

    April 21, 2018
  • Jukwaa la uwezeshaji Wanawake litumike kuinua uchumi wa viwanda Busokelo.

    March 08, 2018
  • Kampuni ya ununuzi wa Kokoa Busokelo yakarabati majengo ya shule.

    February 27, 2018
  • View All

Video

Ujumbe wa Rais
More Videos

Quick Links

  • Watumishi Portal
  • Barua pepe

Related Links

  • Wizara ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mbeya
  • Tume ya Utumishi ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Lwangwa, Tukuyu

    Postal Address: S. L. P. 2, Tukuyu

    Telephone: +255 737 205 318

    Mobile:

    Email: ded.busokelo@mbeya.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2018 Busokelo DC . All rights reserved.