Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya amewataka vijana kujitambua na kufanya shughuli zitakazoweza kuwaingizia kipato.
Hayo ameyasema jana katika ukumbi wa halmashauri wakati wa kukabidhi hundi ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu ambapo kiasi cha Tsh. 92 Milioni kimeweza kutolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kwa makundi hayo.
Mhe. Chalya amesema kuwa vijana bado wana kasumba ya kuelewa kuwa uwezeshaji ni kupewa fedha mfukoni na kwenda kufanya matumizi kitu ambacho si sahihi, bali wanatakiwa kuangalia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kupewa mikopo na kufanya ujasiriamali.
“kwa hiyo mimi nitoe wito kwa vijana, tunapokaa huko kwenye vikundi vyetu na kuilaumu Serikali kuwa tuanakula mlo mmoja… swali ni kuwa hiyo milo mingine unataka nani akuandalie, nendeni mkajitume na mfanye kazi”. Alisema Mhe. Chalya
Mhe. Chalya aliongeza kuwa hili suala la kilalamikia Serikali kuwa haiwajali wakati ikiwajali vijana wanaingia mitini halitakubalika kwani utafika wakati ambapo itaanza kufuatiliwa nguvu kazi ya vijana inatumika vipi.
Halmashauri ya Busokelo imeendelea kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na walemavu kwa kutenga 10% ya mapato ya ndani na kuwezesha makundi hayo ambapo mpaka kufikia robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha 2018/19 imeshatoa jumla ya Tsh. 199,500,000.00 kwa vikundi 57 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli .
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.