Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya amewataka viongozi na Wataalamu wa Halmashuri ya Wilaya ya Busokelo kuwa makini katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ameyasema hayo jana katika mkutano wa baraza la Madiwani la kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2018/19 ambapo amewataka wataalamu kuwa makini na matumizi ya fedha za miradi kwa kutumia “Force Account”.
Mhe. Chalya amesema kuwa wengi wanadhani kuwa utekelezaji wa miradi kwa kutumia akaunti hiyo ni wa holela tu kitu ambacho si kweli, kwani akaunti hiyo kwa kanuni zile zile za fedha ya Serikali na si vinginevyo.
“Force Account.. ni utaratibu wa manunuzi wa kisheria, ….ukisoma sharia ya manunuzi yam waka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 zinaeleza utaratibu mzima wa manunuzi kwa fedha za Serikali”. Alisema Mhe. Chalya
Mhe. Chalya aliongeza kuwa katika kuandaa mahitaji ya utekelezaji wa miradi lazima tushirikiane na TAMISEMI ili kamakunakuwa na mabadiliko ya utekelezaji wa mradi basi taarifa iweze kutolewa ili kuweka hali ya uwazi katika matumizi ya fedha za mradi na kuondoa dhana ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.